John 16:1-6

1 a“Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkaiacha imani. 2 bWatawatenga na masinagogi. Naam, saa yaja ambayo mtu yeyote atakayewaua atadhani kwa kufanya hivyo anamtumikia Mungu. 3 cNao watawatenda haya kwa sababu hawamjui Baba wala mimi. 4 dLakini nimewaambia ninyi mambo haya, ili saa hiyo ikiwadia mpate kukumbuka ya kuwa nilikuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.

Kazi Ya Roho Mtakatifu

5 e“Sasa mimi ninakwenda kwake yeye aliyenituma, lakini hakuna hata aniulizaye, ‘Unakwenda wapi?’ 6 fKwa sababu nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni.
Copyright information for SwhKC